Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob amesema Jumanne wiki ijayo atafungua kesi ya jinai dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana na madai ya kuwa na vyeti feki.
Jacob pia amesema, atamshtaki Makonda katika sekretarieti ya maadili ya utumishi wa umma, tume ya haki za binadamu pamoja na utawala bora.
Amesema kesi hiyo ambayo itaongozwa na mawakili Tundu Lissu pamoja na Peter Kibatara.
“Tunachosubiri ni wanasheria wamalize mchakato wa uchaguzi Chama cha Wanasheria Tanganyika (TSL) na mara watakaporejea kutoka Arusha tutakwenda mahakamani” amesema
0 comments :
Post a Comment