Zanzibar yafutwa Uanachama CAF

Ikiwa ni miezi minne tu imepita tangu Zanzibar ilipopata uanachama rasmi wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) taarifa zinaeleza kuwa uanachama huo umefutwa.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la BBC, ni kuwa Rais wa CAF, Ahmad amesema kuwa Zanzibar ni sehemu ya Tanzania na haikutakiwa kupewa uanachama huo ambapo ilikuwa mwanachana wa 55 kutokana na baadhi ya mambo kukiukwa.
"Walipewa uanachama bila kufuata taratibu zote, Caf haiwezi kukubali kuwa na wanachama wawili ndani ya nchi moja.
"Maana ya taifa inakuja kutokana na kutambulika na Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa (UN)," alisema rais huyo.
Licha ya Zanzibar kukubaliwa uanachama Machi, mwaka huu, upande wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) lenyewe liligoma kuipa Zanzibar uanachama wakati wa utawala wa Issa Hayatou aliyekuwa Rais wa CAF.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment